Taarifa zilizotufikia sasa hivi toka Swedeni ni kuwa Mwili wa marehemu umehamishwa toka Hospitali ya awali alikohifadhiwa na kuamishiwa Hospitali nyingine kwa ajili ya kufanyiwa postmortem. Zoezi hili linakadiriwa kuchukuwa siku tatu mpaka saba.
Taarifa nyingine zitatolewa kadri zinavyopatikana. Wapendwa mnaombwa kufika nyumbani kwa marehemu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili kuwafariji wafiwa.
Aidha tunatoa shukrani kwa wale wote ambao wameshindwa kufika lakini wameweza kutoa rambirambi zao kwa njia ya M Pesa, TiGO Pesa na Airtel Money. Pia hata wewe hujachelewa waweza toa rambirambi zako kwa namba zifuatazo; 0765694533, 0713263556 na 0786027666.(Tafadhali piga simu kabla hujatuma ili uwe na uhakika na unakozituma)
Asanteni Sana. Mungu awabariki
Tunaomba ushirikiano wenu.
Noel Kiunsi
Katibu Mkuu
TUSA
No comments:
Post a Comment