Kuzaliwa 25/12/1970
Katesh – Manyara Zamani Arusha
Shule ya Msingi 1977-1983
Sambaru Shule ya Msingi
iliyoko Singida
Elimu ya Sekondari 1984-1987
Tumaini Shule ya Sekondari- (Singida)
Kidato cha kwanza hadi cha nne
1988-1990 Shule ya Sekondari Sengerema - Mwanza
Kidato cha tano na cha sita
1990 Alijiunga
na jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa sheria (Makuyuni JKT -Arusha)
1991-1993 Mwaka
1991 Marehemu alichaguliwa kujiunga na Chuo cha Ualimu Marangu na kuhitimu stashahada
ya Ualimu mwaka 1993
1993 Aliajiriwa
kufundisha shule ya Sekondari Siha iliyoko Mkoani Kilimanjaro. Alifanya kazi
mpaka 1995.
11/12/1994 Tarehe 11/12/1994 Alifunga NDOA
Takatifu na Bi Dianaeli G. Masaki katika kanisa la TAG Sayuni – Sanya juu
1995 -1999 Mwaka
1995 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na kuhitimu digrii yake ya kwanza ya elimu ya Viungo,
Michezo na Utamaduni (Physical Education, Sports and Culture) mwaka 1999.
1999-2002 Mwaka
1999 alipata nafasi ya kuendelea na masomo Chuo Kikuu cha Dar es salamm akisoma
digrii ya pili ya Elimu (M.A Education) na alihitimu mwaka 2002
2002 Mwaka
2002 Aliajiriwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kama Mkufunzi Mkuu wa Michezo akiwa
chini ya ofisi ya Mshauri wa wanafunzi, Aidha akiwa anashughulika na shughuli
za michezo, marehemu pia alikaimu nafasi ya afisa tawala Ofisi ya Mshauri wa
wanafunzi hadi mwaka 2005.
2006 Mwaka
2006 Marehemu alibadilishwa kazi kutoka kazi ya -Ukufunzi wa Michezo na alijiunga
na Idara ya Elimu ya Viungo na Sayansi za Michezo chini ya Shule Kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha
Dar es salaam akiwa Mhadhiri Msaidizi yaani Assistant Lecturer cheo ambacho amedumu nacho hadi mauti
yanampata.
2011 Novemba
2011, Alijiunga na Chuo Kikuu cha Kristianstad Kilichopo Swedeni kwa ajili
kumalizia masomo yake ya PhD aliyoyaanza mwaka 2005 Chuo Kikuu Huria.
USHIRIKI WA MAREHEMU
KATIKA MICHEZO
1981 -1983- Marehemu alishiriki katika mashindano ya Mbalimbali.
Alishiriki mashindano ya UMITASHIMUTA kwa
ngazi ya Taifa akiwa mshiriki katika mchezo wa mpira wa
miguu na riadha akiwa shule ya Msingi.
1985 -1991 Akiwa shule ya Sekondari Marehemu alishiriki
kwenye michezo ya UMISSETA akiwa
mchezaji wa mpira wa miguu, riadha na mpira wa wavu akiwakilisha kanda ya kati.
Marehemu
alishiriki kwenye michezo ya UMISSETA
kanda ya ziwa akiwa mshiriki katika michezo ya soka na wavu ( Shinyanga na
Tabora)
1991 Akiwa
Jeshini Marehemu alishiriki Michezo ya Majeshi iliyofanyika Arusha akiwa
anacheza mpira wa miguu.
1992-1993 Alichezea timu ya USHIRIKA mkoani Kilimanjaro ikiwa daraja la kwanza.
1996- 1998
Akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu alishiriki katika michezo ya SHIMIVUTA na kukiwakilisha Chuo katika michezo
mbalimbali .
2003 Mwaka
2003 alishiriki michezo ya SHIMMIVUTA iliyofanyika
Arusha akiwa Kocha Mkuu wa timu ya Chuo Kikuu cha Dar es salamm.
2002-2004-2006. Alikua Kocha mkuu wa timu ya chuo
kikuu cha Dar es salaam iliyoshiriki kwenye michezo ya Vyuo vikuu vya Afrika
Mashariki. Iliyo fanyika UDSM, Kenyatta University na Kampala University.
2007 Mwaka
2007 alishiriki Michezo ya Vyuo Vikuu vya Dar es salaam akiwa Kocha Mkuu wa
timu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Tangu 2008- Amekuwa mwamuzi wa mashindano mabali mabali ya
Shirkisho la Riadha nchini
2010 Alihudhuria,
na kufaulu, mafunzo ya ufundishaji (kocha) wa riadha ya vijana kwenye Kituo cha
Maendeleo ya Riadha cha Shirikisho la Duania la Riadha kilichopo Nairobi.
January, 2012 Alichaguliwa kuwa mjumbe wa Chama cha Riadha Mkoa
wa Dar es Salaam
NAFASI NMBALIMBALI
ALIZOSHIKA MAREHEMU
1997-1998 Alikua Mweka Hazina wa Shirikisho la Michezo
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TUSA).
2002-2004 Alikua ni Kocha Mkuu na Mratibu wa shughuli za
michezo Chuo kikuu cha Dar es salaam
2003- 2004 Mwakilishi wa Wafanyakazi wa ofisi ya Mshauri
wa Wanafunzi katika Baraza la Wafanyakazi la Chuo Kikuu cha Dar es salaam
2005 Hadi
mauti yanampata alikua Katibu Mkuu Msaidizi kwenye Shirikisho la Michezo ya Vyuo
Vikuu Tanzania (TUSA).
2011 - Pia hadi mauti yanampata Marehemu alikuwa
Mjumbe wa Halmashauri kuu wa THTU – Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es salaam na
Mwakilishi wa Tawi katika Halmashauri ya THTU taifa.
HUDUMA KWA JAMII
Marehemu amekua akishiriki katika
uandaaji wa matamasha mbalimbali ya michezo ya wafanyakazi, wanafunzi wa Chuo Kikuu
cha Dar es salaam pamoja na mashirika mengine ya umma na binafsi.
Marehemu alijihusisha sana na wanafunzi
wenye ulemavu mbalimbali kwenye suala la michezo, na hilo ndilo lilimpa hamasa
ya kwenda kusoma PHD inayohusiana mambo ya ulemavu
MAREHEMU
AMEACHA MKE NA WATOTO WAWILI.
BWANA
AMETOA NA BWANA AMETWAA,
JINA
LA BWANA LIHIMIDIWE.
No comments:
Post a Comment