Ndugu Wanachama, wana michezo na Watanzania kwa Ujumla.
TAARIFA YA MSIBA WA ALIYEKUWA KATIBU MKUU MSAIDIZI MAREHEMU ANDREA HANGE (1970-2012)
Kwa niaba ya Shirikisho la Michezo la Vyuo Vikuu Tanzania(Tanzania University Sports Association)
Nawataarifu kuwa tulipokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Kiongozi
mwenzetu wa TUSA, Mpendwa wetu Ndg. Andrea Lesso Hange ambaye hadi
kifo chake alikuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa TUSA na Mhadhiri Msaidizi wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kifo chake Kilitokea tarehe 02/03/2012
huko Swedeni alikokuwa
masomoni. Taarifa tulizonazo ni kuwa mwili wake ulikutwa chumbani kwake.
Uchunguzi wa kifo chake bado unaendelea. Taarifa tulizo nazo kama chama
ni kuwa mwili utawasili hapa nchini tarehe 20/03/12 na unatarajiwa
kuzikwa tarehe 21/03/12 Kwa hivi sasa Msiba upo nyumbani kwake Chuo
Kikuu cha
Dar es Salaam Karibu na Hall One. Tunawaomba wanachama wote wa TUSA,
wanafunzi wote waliosoma Elimu kwa michezo nyakati tofauti pale Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, wanamichezo wote na watanzania kwa ujumla
tukutane wote kwa pamoja tarehe 19/03/12 ili kufanikisha shughuli hii.
Watu wote tushirikiane
katika kipindi hiki kigumu kwani mwili umesubiriwa kwa muda mrefu na
gharama zimekuwa kubwa. Pia
unaombwa kutembelea Blog ya TUSA (http://tusadailyblog.blogspot.com/) kwa kupata taarifa nyinginezo kuhusu msiba huu.
Asante Sana kwa Ushiriakiano Wenu
NOEL KIUNSI
KATIBU MKUU TUSA
NOEL B. KIUNSI
PRINCIPAL GAMES TUTOR
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
P.O. BOX 35091
DAR ES SALAAM
TANZANIA
+255713263556
TANZANIA UNIVERSITIES SPORTS ASSOCIATION (TUSA) P.O Box 35091 – Dar es Salaam – Tanzania Tel.No +255-22-2410500/9 Ext: 2004/2018 TelegramUNIVERSITY DAR ES SALAAM Direct Line: 2410256 TeleFax +225-22-2410078 E-mail: tusasports@yahoo.com Website address: www.udsm.ac.tz
HUJAMBO
"KARIBU UJIUNGE NASI KUPATA TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO YA VYUO VIKUU KILA SIKU KUTOKA HAPA NCHINI TANZANIA HIZI NI HABARI ZA MICHEZO AMBAZO ZIMEVIHUSU VYUO VYA HAPA NCHINI IKIWA NI PAMOJA NA USHIRIKI WA VYUO KATIKA MATAMASHA MBALIMBALI KITAIFA NA KIMATAIFA MABONANZA NA MASHINDANO MAKUBWA YA KIMATAIFA YANAYO HUSU VYUO VIKUU, KUMBUKA MICHEZO HUANZIA MASHULENI NA KATIKA VYUO MUENDELEZO NDIKO UNAKOPATIKANA KARIBU SANA"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment